Kakolanya Afunguka Kuhusu Kuvunja Mkataba Yanga

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kakolanya Afunguka Kuhusu Kuvunja Mkataba Yanga
Kipa wa Yanga, Beno Kakolanya ameamua kuvunja ukimya juu ya taarifa zilizozagaa mitandaoni kuwa ameamua kuvunja mkataba na klabu yake.

Kakolanya ambaye amekiri wazi kuwa anaidai Yanga fedha za mshahara wake, amepinga uwepo wa taarifa hizo akisema bado ni mchezaji halali wa Yanga.

Licha ya kuwa anadai, Kakolanya ameonekana kutofurahishwa na taarifa hizo ambazo amezieleza ni za kumlisha maneno bila ya yeye kusema.

"Si kweli kuwa nimevunja mkataba na Yanga, kuna baadhi ya watu wanataka kunichonganisha na klabu yangu, bado nina mkataba na timu, yanayosambazwa hayana ukweli' amesema.

Beno amesalia jijini Dar es Salaam wakati kikosi cha Yanga kiliposafiri kuelekea jijini Mbeya kwa ajili ya mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons itakayopigwa leo Jumatatu.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad