Ndoa Yamfika Hapa Irene Uwoya Aapa Kutoolewa Tena

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ndoa Yamfika Hapa Irene Uwoya Aapa Kutoolewa Tena
KIAPO! Mkali wa filamu za Kibongo, Irene Uwoya ameapa mbele ya Gazeti la Ijumaa Wikienda kwamba hataki tena kusikia kitu kuolewa kwenye maisha yake.

Uwoya alisema kuwa amefikia kwenye uamuzi huo kwani aliyokutana nayo ndani ya ndoa yameshatosheleza moyo wake hivyo kwa sasa yupo kwa ajili ya kuangalia maisha yake na si vinginevyo.



Katika mahojiano maalum na Ijumaa Wikienda, Uwoya alisema kuna vitu vingi anavyo moyoni, lakini pia anaona siyo vyema kuwapa watu faida na ndiyo maana alikuwa anakaa kimya kwa muda mrefu tangu kusambaa kwa habari zake za kuachana na Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’.



HATAKI TENA NDOA?

Uwoya alisema kama ni ndoa, basi ameshafunga mbili ambazo zilimletea shida na sasa haoni sababu tena ya kushobokea ndoa. Mwanamama huyo alisema ameshaonja tamu na chungu hivyo haoni sababu tena ya kujiweka kitanzini.



“Kiukweli kabisa nimeapa moyoni mwangu sitaki kabisa kusikia kama kuna kitu kinaitwa ndoa kwa sababu nahisi hivyo vitu kwenye maisha yangu vimeshapita, sihitaji kuvirudia, naangalia maisha mengine ya kujiendeleza mwenyewe.



“Kama sasa hivi nina kazi kubwa ya kumalizia pub (baa) yangu ya Last Minute (ipo Sinza-Mori, Dar). Kwa hiyo akili yote imeahamia huko,” alisema Uwoya ambaye ni mama wa mtoto mmoja wa kiume, Krish aliyezaa na marehemu Hamad Ndikumana.



ASHAPEWA TALAKA?

Ijumaa Wikienda lilikwenda mbele zaidi na kumuuliza Uwoya kuhusu hatma yake na Dogo Janja na kama alishapewa talaka kutoka kwa jamaa huyo ambapo alisema hajawahi kupewa talaka hivyo hawako pamoja kibububu, lakini maisha yaendelea kama kawaida.



“Sijapewa talaka na Dogo Janja na sijawahi kuacha kumpenda hata siku moja, lakini maisha mengine lazima yaendelee na ndiyo maana nikasema sasa hivi niko bize kufanikisha ndoto zangu nyingi nilizokuwa nimejiwekea kwa muda mrefu.

“Mambo hayo ya kuolewa niwaachie wengine,” alisema Uwoya.



ANATOA WAPI JEURI YA FEDHA?

Hivi karibuni, Uwoya amekuwa akionesha jeuri ya fedha kwa kuvaa nguo za thamani na kutupia kwenye ukurasa wake wa Mtandao wa Instagram.

Mbali na hilo pia hivi karibuni aliangusha sherehe baab’kubwa kwenye boti ambapo aliwaalika marafiki zake hivyo kuzua maswali lukuki juu ya ni wapi anapozipata fedha hizo ambapo alikuwa na haya ya kusema:



“Jamani tatizo la watu wengi wanapenda sana kuwaangalia watu kwa wasiwasi na wengi wanapenda sana kujua mtu anafanya nini au amepata wapi fedha. Sidhani kama ni sawa kuweka wazi kila kitu ambacho mtu anakifanya, kuna wakati mtu unakuwa kimya wao wanaona mambo yako tu yakinyooka,” alisema Uwoya ambaye hakuweka wazi anatoka na nani kimapenzi kwa sasa.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad