Golikipa wa Yanga Klaus Kindoki Afiwa na Baba Yake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Golikipa wa Yanga Klaus Kindoki Afiwa na Baba Yake
Mlinda mlango wa klabu ya Yanga raia wa DR Congo, Klaus Kindoki amempoteza baba yake mzazi ambaye amefariki nyumbani kwao Congo. Klabu imethibitisha.


Kupitia taarifa yake, Yanga imempa pole mchezaji huyo ambaye amejiunga na timu mismu huu wa 2018/19 na tayari ameshacheza mechi kadhaa za ligi kuu soka Tanzania bara.

''Uongozi wa Yanga unatoa pole kwa mchezaji Klaus Kindoki pamoja na familia yake kwa kumpoteza Baba yake. Msiba upo kwao Congo DRC na mazishi yatafanyika siku ya Jumapili uko uko kwao Congo'', imeeleza taarifa ya klabu.



Kindoki alikuwa langoni kwenye mchezo wa ligi kuu kati ya timu yake ya Yanga dhidi ya Mwadui FC ambapo vinara hao wa ligi waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 na kuzidi kujikita kileleni wakiwa na alama 53.



-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad