Kina Zitto Kabwe kwenda Mahakamani sakata la CAG na Spika Ndugai

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe ameeleza kuwa wamepanga kwenda mahakamani kuhusu sakata la Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof.  Prof. Mussa Assad.

Mussa Assad na Spika wa Bunge, Job Ndugai.Zitto Kabwe ameeleza kuwa wamefika uamuzi huo pamoja na wabunge wengine. Kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika;

"Baada ya kushauriana na Wanasheria na Wabunge tumeona ni muhimu sana kwa maslahi mapana ya nchi yetu kulinda Katiba yetu. Baadhi ya Wabunge kutoka vyama vyote tumeamua kwenda mahakamani kuomba tafsiri ya KINGA ya CAG kwa mujibu wa Katiba na mamlaka ya Spika kutoa Wito kwa CAG," ameeleza.

Utakumbuka hapo jana Spika Ndugai alimtaka CAG, Prof. Mussa Assad  kufika mbele ya Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Januari 12 mwaka huu kujieleza kufuatia kauli za kudhalilisha Bunge.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad