1/05/2019

Pichani ni Wafungwa Wawili Tofauti Wanaofanana Waliosababisha Matumizi ya Fingerprint Kutumika


Hii picha ni ya watu wawili tofauti, Wa kushoto jina William West na Wakulia jina William West.

Hawa jamaa wote walikamatwa kwa makosa tofauti na kupelekwa katika gereza moja la Leavenworth, huko marekani mwaka 1903 katika mida tofauti.

Baada ya kufikishwa gerezani , William West wapili, mapokezi wali mshangaa na kusema ,wewe si umeletwa apa gerezani , muda mchache uliopita kwa kosa fulani, inakuwaje sasa unakuja tena hapa. Lakini William West alikataa kuwa sio yeye. Uzuri palikuwa na mafaili walipo angalia faili ni kweli waliona picha na jina hilo hilo. William West aliendelea kukataa sio yeye, ndipo askari walipo amua kwenda gerezani, na chakushangaza walimkuta yule mfungwa alie itwa William West pia, walimtoa na kuwaweka pamoja , na walionekana kufanana kila kitu mpaka jina, kama unavyo ona apo pichani. Inasemekana hawa ndio walio sababisha kuanzishwa kwa *FINGERPRINTS* , kama alama ya utambulisho sahihi mpaka hivi sasa.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger