Serikali: Tundu Lissu alishindwa kujibu maswali ya BBC, aliishia kubabaika tu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Msemaji wa Serikali, Dk Hassan Abbas amemjibu mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) Tundu Lissu, akidai kuwa mwakilishi huyo wa wananchi anazungumza uongo kuhusu maendeleo ya Tanzania.

Dk Abbas amesema kwamba licha ya kuulizwa mazuri ya Serikali lakini Lissu alishindwa kujibu na badala yake aliishia kubabaika.

Akihojiwa na kituo cha Utangazaji Uingereza (BBC) jana Januari 16, 2019, Lissu amezungumza masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na maoni yake kuhusu maendeleo ya nchi, utawala wa katiba na mpango wake wa kugombea urais.

"Unakwenda Ulaya unaponda nchi yako eti haifuati Katiba wakati wewe mwenyewe kuanzia ubunge wako, sifa za ubunge wako na taratibu za uchaguzi wa ubunge wako vyote vipo kwenye Katiba na ndio maana ukawa mbunge,” amesema Dk Abbas.

Dk Abbas amedai Lissu hata alipoulizwa mazuri aliyoyaona licha ya changamoto zilizopo, alishindwa kujibu vyema.

"Angalia alivyoshindwa si tu kueleza jema moja la nchi yake baada ya kupewa fursa hiyo, bali kashindwa hata kueleza jema moja alilofanya yeye binafsi jimboni kwake, kaishia kubabaika tu," amedai Dk Abbas.

Amesema Serikali ya Awamu ya Tano ina dhamira tofauti na ile waliyonayo watu wa aina ya Lissu, hivyo itaendelea kutekeleza wajibu wake katika kuwaletea Watanzania maendeleo ya kweli.

"Sisi tunapigania maendeleo na Watanzania wanaona kazi kubwa inayofanyika kote nchini iwe reli, maji, viwanda, umeme na mambo mengine. Hakuna wa kutuzuia katika kuiletea Tanzania maendeleo. Hakuna,” amesisitiza.

Source: Mwananchi
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad