1/11/2019

Tatizo la kushuka Sukari na Sanona Vyamtesa Mume wa Amber Rutty

Tatizo la kushuka Sukari na Sanona Vyamtesa Mume wa Amber Rutty
Kijana Said Mtoplai ambaye ni mume wa 'video vixen', Amber Rutty, ameweka wazi kile kilichomfanya aanguke mahakamani, na kumpelekea kulazwa hospitali.

Akizungumza na ww.eatv.tv, Said amesema kwamba alinguka mahakamani hapo kwa kuwa hayuko sawa kiafya tangu alipotoka gerezani, na kwa mujibu wa daktari kunachomsumbua ni kushuka kwa sukari na sonona.

“Nashukuru Mungu sijambo hivyo hivyo, hospitali wameniambia tatizo sukari ilikuwa imeshuka na pia nina sonona, mpaka sasa bado nipo hospitali natibiwa”, amesema Said.

Hapo jana Said alianguka akiwa anatoka mahakamani kusikliza kesi yao inayowakabili yeye na mke wake Amber Ruty, ya kusambaa kwa video yao inayowaonesha wakifanya ngono kinyume na maumbile.

Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Janeth Mbando aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 11, 2019 baada ya Wakili wa upande wa mashtaka, Neema Mbwana kusema kuwa upelelezi haujakamilika.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger