Young Killer aivaa ndoa ya Dogo Janja na Uwoya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Young Killer aivaa ndoa ya Dogo Janja na Uwoya
Msanii wa muziki wa Hip Hop nchini, Young Killer 'Msodoki" amefunguka juu ya maneno aliyoyatumia katika wimbo wake wa kama inavyodaiwa kuwa ulilenga ndoa ya Dogo Janja na Irene Uwoya.

Katika wimbo huo, Young Killer ametumia maneno yanayosema, "hata ukinitukana ni kawaida kama hizi ndoa za mabibi na vijana" ambayo wengi wametafsiri kuwa ni 'dis' kwa msanii mwenzake huyo lakini mwenyewe amesema kuwa hakumaanisha hivyo.

Akizungumza katika mahojiano na Friday Night Live (FNL) ya EATV, Young Killer amesema kuwa yale ni maneno tuu ambayo wasanii wa Hip Hop wamekuwa wakiyatumia lakini hayakumaanisha kuwa anamzungumzia Dogo Janja.

"Yale ni maneno tuu ambayo huwa tunayaandika, lakini sijamaanisha kumzungumzia Dogo Janja. Kwanza mimi na Dogo Janja hatuna ugomvi wowote na hatujawahi kuwa na ugomvi, nimezungumza kwasababu ni suala la kawaida tuu sasahivi kwa vijana kuwa na mahusiano na watu wazima".

Pia Young Killer amesema mashabiki wake wategemee kazi kubwa kubwa kwa mwaka 2019 kwani alishaanza kufanya 'Collabo' za kimataifa mwaka uliopita kwa kufanya na Kaligraph Jones pamoja na Dela, wote kutoka Kenya.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad