Baada ya Kumtaja Tundu Lissu,CHADEMA Wampa Masharti Rais

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimemtaka Rais wa TFF Wallace Karia kumuomba radhi Mbunge wake na Mwanasheria Mkuu wa chama hicho Tundu Lissu, bila hivyo wametangaza moja ya mambo watakayofanya ni kuhamasisha wanachama wake kutoshiriki shughuli za TFF.


Chama hicho kimetoa tamko hilo ikiwa ni saa chache baada ya Rais wa TFF kulitaja jina la Mbunge huyo wa Singida Mashariki katika mkutano wa mwaka wa Shirikisho hilo uliofanyika jijini Arusha.

Kwenye taarifa yao CHADEMA wameandika 'chama tumepokea  kauli yenye ukakasi mkubwa iliyotolewa na Rais wa Chama cha Mpira wa miguu Tanzania (TFF) Ndugu Karia kuwa atawashughulikia wale wote ambao wataleta " U-Tundu Lissu" kwenye mpira.

"Sasa kauli ya Karia inatufanya tujiulize maswali mengi kama vile , inawezekana anawajua waliomshughulikia Tundu Lissu na ndio maana anataka kuwatumia kushughulikia 'Tundu Lissu' walioko kwenye mpira"

"Kusimamisha mahusiano na ushirikiano wowote na TFF ikiwemo kuwataka Wanachama wetu kutokushiriki matukio yote yanayoandaliwa na TFF, kususia bidhaa zote zenye nembo au zinazotolewa na TFF zikiwemo jezi za timu za Taifa  na nyinginezo.

"Kuchukua hatua dhidi ya makampuni ambayo yataendelea kushirikiana na TFF ikiwemo kususia bidhaa zao, kwani watakuwa wanaunga mkono taasisi inayoongozwa kwa ubaguzi wa kisiasa, kuwashawishi wadau wa mpira kokote kusitisha mahusiano na TFF kwani inaendeshwa kisiasa na kibaguzi."

"Tunamtaka Ndugu Karia aombe radhi hadharani na aeleze kwa umma kauli yake ilimaanisha nini na kama anaona ni haki kwa Lissu kupigwa risasi na ndiyo njia sahihi ya kushughulikia changamoto za kwenye mpira".
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad