Kimenuka...Dodoma FC Yabambwa Wakitoa Rushwa Kwa Mchezaji wa Rhino Rangers..Wanaswa Wakitoa Fedha

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Viongozi wa klabu ya Dodoma FC wametuhumiwa kutoa rushwa kwa mchezaji wa Rhino Rangers ya Tabora kwa lengo la kusaidiwa kushinda mchezo wao wa ligi daraja la kwanza kundi D.


Mkasa huo umetokea mjini Tabora ambapo viongozi wa Dodoma walimtafuta beki wa Rhino Rangers ambaye jina lake halijawekwa wazi na kukubaliana wampe kiasi cha shilingi elfu 50,000.

Imeelezwa kuwa mchezaji huyo aliwataarifu viongozi wa Rhino na kuweka mtego ambapo waliwanasa viongozi hao wakimkabidhi fedha hizo.

www.eatv.tv imemtafuta RPC wa mkoa wa Tabora ambaye amesema suala hilo halijaripotiwa kwake na huenda limeripotiwa kwenye Mamlaka husika ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ambao tunaendelea kufanya jitihada za kuwatafuta.

Mchezo huo wa ligi daraja la kwanza unachezwa jioni hii kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.

Zaidi sikiliza sauti hapo chini ikieleza zaidi kuhusu suala hilo
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad