Mwasiti Afunguka Chanzo Cha Kuwa Karibu na Godzilla "Mama Yake Alinifata Niwe Karibu na Mwanaye"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwasiti Afunguka Chanzo Cha Kuwa Karibu na Godzilla "Mama Yake Alinifata Niwe Karibu na Mwanaye"
Msanii wa muziki wa kizai kipya, Mwasiti Almasi, ameweka wazi kuwa alishawahi kufuatwa na mama mzazi wa marehemu Godzilla akimtaka amsaidie, ili naye afanikiwe.


Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Mwasiti amesema kwamba kutokana na jambo hilo akawa karibu sana na familia ya Godzilla, na kushirikiana kwenye masuala mbali mbali.

“Ilikuwa benki mjini, Godzilla alikuwa amekuja na mama yake, akaniambia napenda unavyoimba, ningependa pia umshike mkono mdogo wako na yeye aishi katika mazingira mazuri na kufanya kazi, nikamwambia sawa, mama, kuanzia hapo tukawa karibu sana kama familia, tulikuwa tunaongea mambo mengi sana”, amesema Masiti.

Ikumbukwe kwamba Mwasiti ni mmoja wa watu ambao walikuwa karibu sana na Godzilla, na kuweza kufanya kazi pamoja huku wakiwa na mlengo ya kuachia album ya pamoja.

Godzilla amefariki dunia juzi Februari 13, na anatarajiwa kuzikwa kesho Jumamosi, Februari 16 katika makaburi ya Kinondoni

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad