Simba yatua Dar kwa mafungu ikitokea Misri kweye mchezo wa klabu bingwa Afrika dhidi ya Al Ahly

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Simba yatua Dar kwa mafungu ikitokea Misri kweye mchezo wa klabu bingwa Afrika dhidi ya Al Ahly
Baada ya kupokea kichapo kibaya cha jumla ya mabao 5 – 0 dhidi ya Mafarao wa Misri klabu ya Al Ahly mwishoni mwa wiki, hatimaye wawakilishi wa Tanzania Simba SC wameanza kurejea nchini kwa mafungu.


Taarifa kutoka ndani ya klabu ya Simba zinasema kuwa baadhi ya wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wamewasili salama nchini hapo jana Februari 4.

”Baadhi ya wachezaji, benchi la ufundi na viongozi walioambatana na timu nchini Misri wamewasili salama nyumbani Tanzania,” imeripoti klabu ya Simba.

”Mabingwa hao wa ligi kuu soka Tanzania Bara wameongeza ”Wachezaji waliobaki nchini Misri leo (jana) mchana wamefanya mazoezi katika moja ya viwanja vilivyopo kwenye hoteli ya Africana mjini Alexandria. Leo usiku wataanza safari ya kurejea nyumbani Tanzania,”

Kundi hilo la pili limetarajiwa kiwasili leo Februari 5, Mnyama Simba mpaka sasa amepoteza mchezo wake wa pili mfululizo baada ya wakwanza kufungwa 5 – 0 dhidi ya AS Vita Club ya DR Congo ikiwa ni michuano ya klabu bingwa Afrika hatua ya makundi.

Meneja wa klabu hiyo Patrick Rweyemamu amesema sababu kubwa ya timu hiyo kurudi kwa mafungu kulitokana na mabadiliko ya muda wa mechi, kwa sababu hapo awali mechi ilipangwa kuchezwa saa 1 jioni lakini baadaye ikabadilishwa na kupelekwa saa 3 usiku.

“Tulitegemea baada ya mechi kumalizika watu warudi usiku ule ule ili wafike Dar es Salaam siku ya Jumapili na kama wote tulivyopata taarifa tulitegemea mechi ichezwe saa 1 ikaja kubadilishwa ikachezwa saa 3, kwa maana hiyo ratiba ya muda wa kuondoka ilibadilika”

“Kwa hiyo kuna baadhi ya watu wataondoka Jumapili ambao toka awali tiketi zao zilikuwa hazina matatizo na kuna baadhi ya wachezaji wengi wataondoka Jumatatu” alisema Rweyemamu.

Simba inatarajia kucheza mchezo wa marudiano dhidid ya Al Ahaly February 12, 2019 kwenye dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mpaka sasa Simba inaendelea kusalia na alama zake tatu na kushika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa kundi D huku wakiwa wamebakiwa na michezo mitatu ukiwemo mmoja pekee wa ugenini dhidi ya JS Saoura.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad