Wanamuziki Davido na Wizkid Wametuma Meseji Kwa Bongo Flava

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 Arena ipo London ndani ya The 02, mji uliojengeka kwa sanaa na michezo. Shoo ya muziki ndani ya 02 Arena huchukua watu 20,000. Kabla ya Mei 2018, haikufikiriwa kuwa 02 Arena ingeweza kujazwa na msanii kutoka Afrika.

Mastaa waliokuwa wakifanya mafuruko ya watu 02 Arena ni Wamarekani na Waingereza, tena mastaa hasa. Na rekodi zinaonesha 02 Arena ina mishemishe kuliko Madison Square Garden, New York.

Oktoba 21, 2017, Wizkid alikuwa msindikizaji kwenye shoo ya rapa wa Atlanta, Georgia, Future. Shoo ilifunga watu kama kawaida ya 02 Arena. Ilikuwa sehemu ya ziara ya Future, Hndrxx tour.

Wizkid akajiuliza kwa nini asiweze? Mei 26, mwaka jana, akaipeleka Afro Republik 02 Arena. Wakaubeza msuli wake. Nini kilitokea? Si mnaita Sellout? Wizkid aliuza tiketi zote kabla ya shoo.

Davido alimpongeza Wizkid kwa maajabu aliyofanya, halafu akajiuliza kama homeboy wake ameweza, nini kimshinde? Januari 27, mwaka huu, Davido aliifanya 02 Arena ifurike.

SMS ni hii; Wanigeria wanaandika historia. Kwenda Uingereza kupiga shoo ni kitu cha kawaida. Kujaza 02 Arena si tukio la kuelezewa kwa maneno ya uzani mwepesi.

Wizkid na Davido hawajichukulii poa. Wanajiona wanaweza kufanya mambo makubwa Ulaya na wamethibitisha. Mfano, mauzo ya tiketi kwa shoo ya Davido bei ya chini ilikuwa pauni 40, Sh122,000.

Ukichukua bei ya Sh122,000 kama kiingilio cha watu 20,000, majibu ni kwamba shoo hiyo imeingiza zaidi ya Sh2.4 bilioni. Hesabu ya chini kabisa.

Wana Bongo Fleva wachukue ujumbe. Waote ndoto kubwa. Waache majungu na kutengeneza timu zisizojenga. Wafikirie matokeo makubwa.

Muhimu ni kusaidiana, kuoneshana njia. Umepiga shoo sehemu unampa pande mwenzako. Umefanya mchongo unaolipa, muunganishe mwenzio. Davido hutembea chini ya falsafa ya "We raise by lifting others." Tunanyanyuka tukiwanyanyua wengine.

Huwezi kunyanyuka ukipambana wengine wasinyanyuke. Utatumia muda mwingi kuzuia wengine badala ya kuongeza kasi ili kufikia malengo. Kwa timu zenu wana Bongo Fleva za kutukanana mitandaoni na kujaziana dislikes au kuchawiana YouTube ili viewers wasiongezeke, hamtafika mbali. Kwanza wengine wanajiona wamefika wakati bado.

Ndimi Luqman MALOTO 
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad