2/03/2019

Yondani Atajwa Kuimaliza Simba ...Mechi ya Yanga SimbaKOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema hana mashaka na wapinzani wake wa Ligi Kuu kutokana na aina ya wachezaji alionao kuwa na uwezo wa kupindua matokeo muda wowote na kuwataja wachezaji ambao wanampa kiburi cha kuutafuta ubingwa.Yanga leo watakuwa Uwanja wa Mkwakwani Tanga wakicheza na Coastal Union wakiwa ni vinara wa Ligi Kuu baada ya kujikusanyia pointi 53 wakiwaacha Simba kwa pointi 20 huku Simba wakiwa na viporo sita kuwa sawa na Yanga kwa sasa.Endapo Yanga watafikia lengo lao wataipindua Simba kimataifa kwenye mashindano yanayoandaliwa na Shirikisho la Mpira Afrika (Caf) ambayo kwa sasa Simba ndiye mwakilishi kwenye mashindano hayo.Akizungumza na SpotiXtra, Zahera alisema, timu nyingi Ligi Kuu zinaichukulia poa Yanga hali inayompa faida ya kuibuka na ushindi kwani mchezo wa mpira unahitaji nidhamu.“Wengi ambao tunacheza nao wanaichukulia poa timu ya Yanga kutokana na kushindwa kufanya usajili wa kutisha hali inayowafanya watuchukulie ni timu ya awaida hicho ndicho kinawaponza
tunawachapa hata wakianza wao kutufunga.“Timu nyingi zinasahau kwamba nina wachezaji wanaocheza timu ya Taifa na wanategemewa sasa hao ndio ambao wananifanya nipate matokeo mchezaji kama Kelvin Yondani, Vincent Dante,Feisal Salum na Gadiel Michael,” alisema Zahera
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger