Lionel Messi Anataka Kuhamia Ligi Kuu ya Marekani

Lionel Messi Anataka Kuhamia Ligi Kuu ya Marekani
Mshambualiaji wa kimataifa wa Argentina anayekipiga katika club ya FC Bacrelona ya Hispania Lionel Messi inahisiwa kuwa inawezekana atakapotaka kumaliza soka lake atahama kabisa bara la Ulaya na akaenda kucheza soka nje ya Ulaya.


Tetesi hizo za Lionel Messi kuwa mbioni kwa miaka ya baadae kwenda kucheza Ligi Kuu ya Marekani MLS zimekuja kutokana na kiungo wa Atlanta ya Marekani Pity Martinez kueleza kuwa ameulizwa na Lionel Messi kuhusu Ligi Kuu ya Marekani kauli ambayo imetafsiriwa kama kuanza kwa uchunguzi wa staa huyo.


Kauli hiyo aliiweka wazi Martinezi akihojiwa na TyC Sports“(Messi) ameniuliza kuhusiana na Ligi Kuu ya Marekani (MLS) kwamba kuna nini kinaendelea” Lionel Messi na Pity Martinez kwa sasa wote wapo pamoja katika kambi ya timu yao ya taifa ya Argentina kwa ajili ya mechi za kimataifa zilizopo katika kalenda ya FIFA.


HABARI HIZI ZINAPATIKA UDAKU SPECIAL APP BONYEZA HAPA UWE NAYO KWENYE SIMU YAKO

Loading...

Lionel Messi Anataka Kuhamia Ligi Kuu ya Marekani Lionel Messi Anataka Kuhamia Ligi Kuu ya Marekani Reviewed by Udaku Special on March 23, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.