Lowassa Afunguka "Msinilishe Maneno Nimerudi Nyumbani Basi"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Na. Alphonce Kusaga, Arusha

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amewaomba Watanzania waliompigia kura katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka 2015 kumuunga mkono, Rais wa Tanzania, John Magufuli.

Lowassa aliyekuwa mgombea Urais katika uchaguzi huo kupitia Chadema na kuungwa mkono na vyama washirika vya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vya NLD, NCCR-Mageuzi na CUF alipata kura milioni sita huku Dk John Magufuli wa CCM akipata milioni nane.

Hata hivyo, Lowassa ambaye alijiunga na Chadema Julai 28, 2015 akitokea CCM, Machi Mosi 2019 alitangaza kurudi CCM.

Leo Jumamosi, Machi 9, 2019 Lowassa amekwenda Monduli mkoani Arusha ambako anakabidhiwa kadi ya uanachama na amezungumza na mamia ya wanachama waliojitokeza kumpokea.

"Nimerudi nyumbani msiniulize nimerudi kufanya nini, nimerudi nyumbani,” amesema Lowassa ambaye amesindikizwa na mke wake, Regina na mwanaye Fred.

Akiendelea kuzungumza amesema, “Kwenye uchaguzi nilipata kura zaidi ya milioni sita si haba, naomba wote walionipigia kura tumuunge mkono Rais John Magufuli.”

"Nampongeza Rais John Magufuli kwa ushawishi wake ambao umenifanya nimerudi nyumbani,"amesema.

Huku akishangiliwa, Lowassa amesema, “Kwa Chadema nawashukuru viongozi na wanachama sana, sitaki watu wengine waniwekee maneno mdomoni.”
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad