Mabantu wafunguka kuhusu Whozu kukatwa nywele

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Twaah kutoka katika kundi la Mabantu, amefunguka kuhusiana na ukaribu  wao kama kundi na Whozu pamoja na skendo ya msanii huyo kukatwa nywele.

Twaah amesema Whozu ni mtu wa karibu sana kwao na hata katika kushauriana masuala madogo madogo wamekua wakipeana kampani kwanamna moja ama nyingine.

Alipoulizwa kuhusiana na skendo ya Whozu kukatwa nywele na kufumaniwa na aliyedaiwa kuwa ni mpenzi wa mwanadada Tunda, amesema kuwa hayuko tayari kujibu swali kama hilo na kuomba liachwe lilivyo.

Hivi karibuni Whozu alikubwa na sakata la ugomvi na mwanaume aliyedaiwa kuwa ni mpenzi wa Video Vixen na mwanadada maarufu mtandaoni, Tunda kutokana na sababu za kimapenzi, hali iliyopelekea Whozu kukatwa nywele zake za kichwani.

Pia amezungumzia kolabo yao pamoja na Whozu kuwa imesaidia kwa kiasi kikubwa kupeleka muziki wao sehemu flani na pia Whozu ni mtu wa karibu sana kwao kimaisha ya kawaida.

"Usije kushangaa kuna kolabo kati ya Whozu na Mabantu panapo majaliwa, mwakani 2019 ni mwaka wa kolabo’’, amesema Twaah.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad