Samatta: TFF Muangalieni Kapombe Katika Zawadi Isipowezekana Nitagawana naye Nusu kwa Nusu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

TFF Muangalieni Kapombe Katika Zawadi Isipowezekana Nitagawana naye Nusu kwa Nusu
Kapteni wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Ally Samatta, amesema yupo tayari kugawana nusu kwa nusu zawadi na beki Shomari Kapombe, endapo kama jitihada za kumpatia zawadi kama wachezaji wengine wa timu ya taifa zitashindikana.

Samatta ametoa ahadi hiyo leo, Machi 26, 2019 ikiwa ni siku moja imepita tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh John Magufuli alipotangaza kuwazawadia viwanja wachezaji walioiwezesha Taifa Stars kufuzu kwenye michuano ya AFCON 2019.

Katika ukurasa wake wa Twitter, Samatta ameandika kwamba "Kama Kaptein ningeomba TFF imuangalie Shomari Kapombe katika zawadi ambazo wachezaji watapata. Ikishindikana basi ningeomba wachezaji wote tumchangie kidogo kidogo".

Ameongeza "Endapo vyote visipowezekana kabisa basi katika ahadi ya Mh Paul Makonda, nitagawana naye nusu kwa nusu".

Mh. Paul Makonda na kamati yake ya 'Saidia Taifa Stars ishinde', waliahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni 10 kwa kila mchezaji wa timu ya taifa endapo watafuzu AFCON jambo ambalo limetimia.

Kapombe alipata majeraha akiwa mazoezini Afrika Kusini siku chache kabla ya kuwakabili Lesotho Novemba 18, 2018.

Tanzania imefuzu fainali hizo zitakazofanyika mwezi Juni huko Misri kwa kuifunga Uganda mabao 3-0 kwenye mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa taifa Dar es salaam, Machi 24, 2019.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad