Unaambiwa Mbwana Samatta Anakimbizana na Messi Katika Magoli Ulaya...Mbappé Akalishwa Chini

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samatta, ameendelea kuwa king'ang'anizi barani Ulaya akiwa ameshafanikiwa kufunga mabao 29 katika michuano yote msimu huu huku akizidiwa na Lionel Messi pekee.

Samatta msimu huu amekuwa kwenye moto akiwa kinara wa ufungaji katika ligi kuu ya Ubelgji akiwa ameweka kambani mabao 20 katika mechi 26 alizocheza.

Mabao mengine 9, ameyafunga katika michuano ya Kombe la Ubelgiji pamoja na Europa League msimu huu hivyo kuwa miongoni mwa wafungaji bora msimu huu mpaka sasa.

Messi ambaye ana magoli 25 kwenye La Liga ndio kinara mpaka sasa akiwa na jumla ya goli 33. Mchezaji Cristiano Ronaldo ambaye kwa misimu kadhaa amekuwa akikimbizana na Messi, ana mabao 21 mpaka sasa.

Habari njema ni kuwa kocha wa taifa Stars Emmanuel Amunike kesho Ijumaa Machi 8, 2019 atatangaza kikosi kitakacho vaana na Uganda kwenye mchezo wa kuwania kufuzu AFCON 2019 hapo Machi 24.

Orodha ya Vinara wa mabao Ulaya

Messi - 33
Samatta - 29
Mbappé - 29
Lewandowski - 27
Piatek - 26
Tadic - 25
Aguero - 25
Luuk De Jong - 24
Dabbur - 24
Bruno Fernandes - 23
Cavani - 22
Kane - 22
Ben Yedder - 22
CR7 - 21
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad