Ticker

6/recent/ticker-posts

Zari Azua Hofu na Drip sita Kitandani, Asema Shetani Muongo

Nafasi za Ajira Serikalini Zilizotangazwa Wiki Hii Bonyeza HAPA

Nafasi za Internship Zilizotangazwa Bonyeza HAPA

Matokeo ya Form Four 2022 Bonyeza HAPA


Zari The Boss Lady amewapa wakati mgumu mashabiki wake kwa kuweka picha za nyakati ambazo sio za ‘bata’ bali nyakati za kupambana na changamoto ya afya yake akiwa kitandani.

Jana kupitia Snapchat, aliweka picha inayoonesha drip na mkono wenye sindano inayomsaidia kuingiza maji mwilini akiwa kitandani na kuwaelezea wafuasi wake kuwa anapambana na ugonjwa ambao umemlazimu kuwekewa drip sita za maji.

“Ninaumwa sana, lakini shetani anadanganya,” tafsiri ya ujumbe wa Kiingereza aliouandika Zari kwenye picha aliyoweka Snapchat.

Hata hivyo, baada ya muda na kuzingatia hofu na jumbe zilizotiririshwa na mashabiki wake kutaka awaeleze kulikoni, aliwaondoa hofu kwa kuweka picha inayomuonesha akiwa kitandani bila drip na kuelezea kinachomsibu.

“Nitakuwa sawa, ni tonsils mbaya tu, homa, maumivu ya kichwa na maambukizi katika kifua,” aliandika kwenye picha hiyo.




Zari ameelezea matibabu yake kuwa aliwekewa drip zote wikendi, ikiwa ni tatu Jumamosi na nyingine tatu Jumapili.

Mrembo huyo kutoka Uganda ni mmoja kati ya watu wenye wafuasi wengi watiifu kwenye mitandao ya kijamii Afrika Mashariki, ikiwa amewahi kuwa maarufu Uganda na kuongezea zaidi umaarufu wake Tanzania na Kenya baada ya kuishi na kuzaa watoto wawili na Diamond Platinumz.

Hivi sasa ana wafuasi zaidi ya milioni 5 na laki moja kwenye Instagram pekee.

Tunamtakia nafuu ya haraka, aendelee kuwapa furaha familia yake na wafuasi wake kwenye mitandao ya kijamii.

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Tanzania Zipo HAPA

Ufadhili wa Masomo ( Scholaships) Bonyeza HAPA

Post a Comment

0 Comments