DRC Waendelea Kuangamia na Ebola,WHO Kutoa Tahadhari Kimataifa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

DRC Waendelea Kuangamia na Ebola,WHO Kutoa Tahadhari Kimataifa
Shirika la Afya Duniani WHO wanafanya tathmini kubaini iwapo mlipuko wa sasa wa ugonjwa wa Ebola ambao umeua mamia ya watu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo unapaswa kutangazwa kuwa hatari ya kimataifa au la.

Msemaji wa WHO, Tarik Jasarevic amesema wataalamu hao wanachunguza hasi na hatari ya ugonjwa huo kusambaa kimataifa. Profesa Robert Steffen wa jopo la wataalamu wa afya wa UN anatazamiwa kutoa tangazo hilo.

Wakati huohuo, watu wanne zaidi wameripotiwa kupoteza maisha kutokana na mlipuko wa Ebola huko Kongo DR. Vifo hivyo vipya viliripotiwa  katika maeneo ya mashariki mwa nchi.

Siku chache zilizopita, Wizara ya Afya ya Kongo DR ilitangaza kuwa, katika muda wa wiki tatu zilizopita, ugonjwa wa Ebola umeua zaidi ya watu 100; na zaidi ya watu 700 wamefariki dunia tangu mwezi Agosti Mosi mwaka jana kutokana na ugonjwa huo hatari.

Kwa mujibu wa takwimu za WHO, tangu homa ya Ebola iliporipuka nchini humo mwezi Agosti mwaka jana 2018 hadi sasa, idadi ya watu waliothibitishwa kuambukizwa au wanaoshukiwa kuambukizwa imefikia 1,206 , na 764 kati yao wamefariki dunia.

Shirika la Afya Duniani limetahadharisha kuwa, mlipuko wa ugonjwa hatari wa Ebola unasambaa kwa kasi nchini Kongo DR, ikiwa ni miezi minane sasa tangu ulipoanza kugunduliwa tena kwa mara ya pili.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad