Rais Magufuli Amtaka Waziri Kutumia Bangi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Rais Magufuli amtaka Waziri kutumia bangi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemtaka Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Makame Mbarawa kuwa mkali ikibidi kutumia kilevi cha bhangi, ili aweze kuwawajibisha watu zaidi.


Rais Magufuli ametoa rai hiyo leo akiwa Makambako Mkoani Njombe ambako anaendelea na ziara yake, na kugusia sekta ya maji ambapo ndipo alipomtaka waziri kutumia kilevi hicho ambacho ni kinyume na sheria za nchi, ili aweze kuwa mkali zaidi.

"Nimekupeleka pale ukafanye mabadiliko, ukalisimamie hilo, kwa sababu nina matatizo sana na baadhi ya miradi ya maji, na ndio maana nimekuwa nikifanya mabadiliko kwenye miradi ya maji, kwa sababu haileti impact.  Zinazungumzwa fedha zimeenda kwenye miradi lakini hazikuenda, kuna wakati nilienda kanda ya ziwa, mradi umetumika milioni 400, zilikuwa milioni 800  lakini maji hayapo, sasa nikuombe Waziri na watendaji mkawe wakali kweli kweli, kama unaweza ukavute bangi ya Njombe ili uwe mkali kaivute, kaivute kisiri siri wasikuone ukiivuta, ili ukienda kwenye mradi hawa mainjia wa maji wakafanye kazi”, amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli bado yuko mkoani Njombe akiendelea na ziara yake aliyoanzia mkoani Mtwara, ambapo amezindua miradi mbali mbali ikiwemo ya barabara, vituo vya afya na viwanda, huku akiendelea kuwataka Watanzania kuchapa kazi.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. vyombovya habari zisivyoelewa mila za au historia ya njombe kuhusiana na maswala ya bangi, ndo vitaitumia kauli hiyo ya utani kuuza habari au kupotosha watu mbalimbali popote walipo.

    ReplyDelete

Top Post Ad