Waziri wa Ulinzi wa Sudan Aapishwa Rais wa Mpito

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Waziri wa Ulinzi wa Sudan Aapishwa Rais wa Mpito
Waziri wa ulinzi wa Sudan Awadh Ibn Auf ameapishwa kuwa Rais wa baraza la mpito la kijeshi ambalo kulingana na Jeshi litaongoza kwa kipindi cha miaka miwili ya mpito.

Kituo cha Redio kinachomilikiwa na Serikali kimearifu kuwa Mkuu wa Majeshi Kamal Andel-Marouf ameapishwa kuwa makamu wa rais wa baraza hilo.

Hatua hii imekuja huku waandamanaji wakilalamika kwamba utawala huo wa kijeshi haukumaanisha mabadiliko, na kuahidi kuendelea kuandamana hata baada ya hapo jana kutangazwa kwa sheria inayozuia raia kutembea Usiku wa kuanzia saa 4 hadi saa 10 alfajiri.

Rais Omar al Bashir wa Sudan aliyetawala kwa miaka 30, jana Alhamisi alipinduliwa na kukamatwa kufuatia miezi kadhaa ya maandamano ya kuipinga serikali. Rais Omar al-Bashir aliyetawala Sudan kwa miaka 30 amepinduliwa na kukamatwa baada ya miezi kadhaa ya maandamano makubwa yaliyoipinga serikali.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad