5/12/2019

Askofu Kakobe afunguka kuhusu RC Makonda, 'ana upungufu tunamsaidia sasa'Askofu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe ameeleza kwanini wiki iliyopita walimuita Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwenye ibada.

Akizunguza leo katika Kanisa la Ufufuo na Uzima kwa Askofu Josephat Gwajima katika sherehe za miaka 30 ya kanisa hilo, Askofu Kakobe amesema walimuita kwa sababu wao ni wazee na wanaweza kumsaidia.

"Tulimleta Makonda kwa sababu sisi ni wazee wa Taifa, kama Makonda ana upungufu tunamsaidia sasa tukimtenga tutamsaidiaje. Tutaendelea kushirikiana naye, tunawapenda watu wote," ameeleza Askofu  Kakobe.

Ameendelea kwa kusema "Wapo wengi walichukia kwanini tulimwalika Paul Makonda katika sherehe za miaka 30 ya kuadhimishwa kwa kanisa langu, Wengine walichukia zaidi baada ya Gwajima kukumbatiana na Makonda"
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger