Mhasibu UDART Afunguliwa Mashtaka 36 ya Kughushi Tiketi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mhasibu wa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka Dar es Salaam (UDART), Alphonce Kika (29), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa akikabiliwa na mashtaka 36 ya kughushi tiketi zenye namba tofauti tofauti za mabasi ya mwendo kasi.

Mshtakiwa Kika anayeishi Mabibo, Loyola amesomewa shtaka lake leo Aprili 30, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde wa Mahakama hiyo na kusomewa mashtaka 36 ya kughushi.

Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali, Janeth Mugho akisaidiana Jenifa Masue amedai, mshtakiwa ametenda makosa hayo Aprili 4, 2019 katika Kituo cha mabasi ya mwendo kasi kilichopo Mbezi ndani ya Wilaya ya Ubungo na jijini Dar es Salaam.

Imedaiwa siku ya tukio mshtakiwa Kika kwa nia ya kudanganya au kutapeli alighushi tiketi 36 za basi zenye namba tofauti tofauti za Aprili 18, 2019 akidanganya kuwa zimetolewa na UDART kitu ambacho si kweli.

Hata hivyo, mshtakiwa amekana mshtaka yote na amerudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana amhapo mahakama imemtaka kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini bondi ya Sh milioni 20. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 13,2019, kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad