Serikali Yaanza Ukarabati Mkubwa wa barabara ya Dar es salaam,Morogoro hadi Dodoma

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Serikali imesema imeanza ukarabati wa mashimo na kupanua barabara ya Dar es salaam,Morogoro hadi Dodoma ambayo ni kiungo muhimu kwa uchumi wa tanzania.

Naibu waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe,Elias Kwandikwa amebainisha hayo Juni 20,2019 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la  mbunge wa Wingi Juma Kombo aliyehoji serikali ina mpango gani wa kukarabati mashimo  pamoja na kuipanua barabarahiyo.

Katika Majibu Yake Naibu waziri wa ujenzi ,uchukuzi na mawasiliano Elias Kwandikwa amesema Serikali  imeanza     ukarabati   mashimo  na   kupanua  barabara   ya   Dar eS Salaam,Morogoro  hadi Dodoma  ambayo ni kiungo muhimu kwa uchumi  Wa Tanzania ambapo mkataba  wa kazi ya upanuzi wa madaraja ya Kibamba,Kiluvya na Mpiji ulishasainiwa tangu tarehe 13,Julai,2018 na  mkandarasi ESTIM Construction.Co.Ltd kwa  gharama ya Sh.Bil.440,Mil.449 ,laki  5 na 21elfu.

Aidha,Mhe.Kwandikwa amesema Ukarabati wa maeneo yaliyoharibika unafanyika kwa kuondoa lami  ya zamani  na kuweka tabaka jipya  katika  maeneo ya Kibaha   hadi  Chalinze  ambapo  mkoa wa Pwani imetenga Tsh.Bil.2.5.

Hata hivyo Serikali imetenga Tsh.Milioni 800 katika mwaka wa Fedha 2018/2019 ili kufanya upembuzi yakinifu  na usanifu wa kina  kwa ajiliya ukarabati  Barabara ya  Morogoro  -Dodoma [km 256]

Katika  hatua nyingine   Mhe.Kwandikwa  amesema mkandarasi yeyote atakayechelewesha kazi atachukuliwa hatua na lipia gharama za usumbufu ambapo kuna mashauri 20 ya Makandasi waliofanya uzembe
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad