Kigwangalla Amesema Atakwenda Kufuatilia Kwa nini Mtoto wa Faru John Kupewa Jina la Kiislamu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla, amesema atakwenda kufuatilia mtoto wa Faru John kama amezaliwa muislamu ama amebadili dini wakati wa kuoa kwa wazazi wake.


Kigwangalla aliyasema hayo leo kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter, kuwa kuna watu wanahoji ni kwa nini mtoto wa faru John anaitwa Faru Rajabu.

Faru John ni mnyama ambaye alikufa baada ya kukosa matibabu alipougua na kuacha mtoto Faru Rajabu.

Mtoto huyo leo amezua gumzo katika mitandao ya kijamii huku wakihoji iweje aitwe Faru Rajabu wakati ametokea kwa uzao wa Faru John.

Faru Rajabu ni kivutio katika hifadhi ya Serengeti kutokana na taarifa zake za hivi karibuni kupongeza mnyama huyo kwa kuongeza idadi ya Faru wengi katika hifadhi huyo.

Waziri Kigwangalla aliandika ujumbe unaosomeka kuwa :”Kuna watu wanahoji ni kwa nini mtoto wa Faru John, Faru Rajabu amebadili dini; bado nafuatilia ni kwamba alizaliwa akiwa muislam, ama amebadili dini wakati wa kuoa! Nitawajuza,”
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad