Hatimaye Lionel Messi aomba radhi kutokana na matamshi yake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Taarifa kutoka Amerika ya Kusini kuwa Lionel Messi ameliomba radhi Shirikisho la soka la bara hilo kufuatia tuhuma za rushwa alizozitoa kwa waamuzi wakati wa michuano ya Copa America.

Hiyo ni kwa mujibu wa Chama cha soka cha Argentina (AFA) ambacho wamepeleka nyaraka kwenye kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Soka Amerika ya Kusini.

Nyaraka ambazo wamepeleka zimeambatanishwa na nyaraka nyingine wakisema zimeandikwa na Messi akiliomba radhi Shirikisho la Soka la Amerika ya Kusini kutokana na tuhuma ambazo alizizungumza baada ya mchezo wa nusu fainali dhidi ya Brazil na baada ya kuoneshwa kadi nyekundu kwenye mechi ya Copa America kutafuta mshindi wa tatu.

Chama cha soka Argentina kimesema Messi ameomba radhi na wanaomba uchunguzi uliokuwa unaendelea kutokana na tuhuma ambazo alizotoa Messi usitishwe badala yake wamuadhibu wakizingatia kuwa tayari Messi ameshaomba radhi wakiamini adhabu yake inaweza kuwa faini au adhabu nyingine ndogo ukilinganisha na ambayo imeshatoka.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad