Hii ndio idadi ya watu waliokufa kwa Homa ya dengue

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema homa ya dengue imeua watu 13 nchini huku 6,677 wakiugua ugonjwa huo.

Takwimu hizo zimetolewa leo na Ummy Mwalimu katika uzinduzi wa mkakati wa Taifa wa kupambana na mbu na wadudu wengineo katika viwanja vya Mnazi Mmoja.

Waziri huyo amesema awali takwimu zilionyesha vifo sita  lakini Serikali ilifanya tathmini upya na kupata takwimu sahihi.

"Tulikuwa na takwimu za vifo sita lakini Serikali tumefanya tathmini upya na kupata idadi ya vifo 13 nchi nzima na Mkoa wa Dar es Salaam ndiyo unaongoza kwani umekuwa na wagonjwa 6,631 na vifo 11," amesema.

"Homa ya dengue ilipoingia watu wakapata taharuki kubwa , mikakati mipana ya kupambana na dengue ikapangwa, lakini ikaonekana bado kuna tatizo kwa kuwa takwimu za Malaria nchini zinaonyesha watu milioni  5.6 milioni wanaugua kila mwaka na vifo 4,390.”

Aidha amesema ugonjwa huo kwa sasa unapungua kwa maelezo kuwa Juni, 2019 kulikuwa na wagonjwa 536 na tangu kuanzia Julai hadi leo kuna wagonjwa sita pekee.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad