Jengo jipya la tatu JNIA kuanza kutumika mwezi ujao

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

NAIBU Waziri  wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano(Sekta Uchukuzi na Mawasiliano),  Mhandisi Atashasta Nditiye, amesema ujenzi wa jengo la  tatu la abiria wa kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA),  kinatarajia  kukamilika mwanzoni mwa Agosti  mwaka huu kwa kuanza kuhudumia abiria

 Amesema amefurahishwa  kwa  kukamilika  kwa ujenzi wa kiwanja hicho  ambapo kwa  vimefungwa vifaa vya kisasa.

 Akizungumza mara  baada ya ziara ya kukagua kiwanja hilo, amesema  kuwa katika idadi ya miruko ya ndege Barani Afrika  inachukua nafasi ya tano  na nafasi ya sita kwa abiria.

‘’ Nimefurahishwa kwa kukamilika kwa ujenzi wa jengo la tatu la abiria wa  kiwanja cha Ndege ambapo utakapoanza kuhudumia abiria natarajia tutachukua nafasi mzuri zaidi Barani Afrika kwani ni kiwanja cha kisasa nahuduma zetu ni mzuri,’’ alisema.

Nae Mkurugenzi  wa Kiwanja cha Ndege cha Mwalimu Julius Nyerere( JNIA),  Paul  Rwegasha, amesema  kukamilika kwa jengo hilo litaweza  kuhudumia  jumla abiria milioni nane kwa mwaka.

Rwegesha alisema  ujenzi wa jengo la kwanza lina uwezo wa kuhudumia abiria 500,000 kwa mwaka na ujenzi wa pili abiria  milioni 1.5

Alisema kukamilika kwa Jengo la tatu la abiria  litaongeza idadi ya ndege, abiria pamoja na watalii baada ya kuwa na miundombinu  bora na yakisasa.

Vile vile alisema ujenzi wa kiwanja cha tatu ni kwa ajili ya abiria wa safari za Kimataifa ambapo kwa sasa yako mashirika na Kampuni 20 na kiwanja cha  pili kwa ajili ya abiria wa safari za   ndani ya nchi na Kimataifa  ambapo yana Kampuni sita  huku kiwanja cha kwanza  safari za  ujumla za ndani ya nchi Kampuni ni  12.

Alisema ujenzi wa jengo la tatu la abiria  litakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria 2,800, kwa saa na maegesho ya magari mchanganyiko yasiopungua 2,075 kwa wakati mmoja.

Mkurugenzi Mkuu wa  Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini(TAA), Mhandisi Julius Ndyamukama, alisema wako katika maandalizi ya wakuu wanchi na Serikali watakaohudhuria mkutano wa 39 wa SADAC  ambapo maadalizi yameambatana na ukarabati wa maboresho ya miundombinu  na samani katiaka jengo  la pili la Abiria.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad