Kubenea Ataka Wanaosambaza Mawasiliano ya Simu ya Nape, Makamba, Kinana Wachukuliwe Hatua

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea ameitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano nchini (TCRA) kutoa taarifa za waliohusika kudukua mawasiliano ya simu ya mbunge wa Mtama, Nape Nnauye na watu wengine.

Wiki iliyopita sauti fupi za mazungumzo ya simu yanayomhusisha Nape, aliyekuwa Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba na makatibu wakuu wastaafu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii

Akizungumza na vyombo vya habari  jana  Julai 22, Kubenea alisema kitendo kilichofanyika ni kinyume cha katiba na sheria za nchi ambazo zinatoa uhuru wa faragha kwa mtu.

“Hii ni hatari sana kama viongozi wanafanywa hivi kwa mambo ya faragha kutolewa si hata baadaye watu wanaweza kuvunja ndoa za watu, kama Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amezungumza na hawara kwa mfano ikatoka nje si jambo la hatari hili, kuna vitu ambavyo vinatakiwa kuwa na usiri kwa maana kama hawa ni viongozi tu je wananchi wa kawaida inakuaje..?

"Haya mambo hayawezi kufanyika katika nchi inayojali utu wa mtu. TCRA itoe taarifa, ni nani aliyefanya kazi hiyo chafu." Alisema

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kubenea Umeenea.
    Nani kakwambia ya npe.
    Mbona ummuanda wa Mtama.
    Au ndiyo unamuwajibisha ki aina...!!!
    usiendelee kumu umbua.. wiki hii yeye
    mwenyewe kistaarabu muulize stivu nilele atakujuuza exlusive .
    Kwa kuludi shaba kulima kolosho si aibu

    ReplyDelete

Top Post Ad