7/11/2019

Mashabiki wamshambulia Nandy mtandaoni, Kisa Hiki Hapa

Mashabiki wa Msanii wa Muziki, Nandy wamemshambulia na kumtaka ageukie mzuki wa Injili baada ya kufanya Cover ya Wimbo wa Joel Lwaga unaoitwa 'Mimi ni wa Juu'.

Nandy amesema kuwa anampenda sana Mungu na nimuumini mzuri sana wa kanisani ipo siku atafanya wimbo wa Gospel na kuwabariki wengi.

"Jamaaaan dm zenu naziona na simu zenu nimepata na comment zenu pia nimesoma jamani me nampenda sana MUNGU na me ni muumini mzuri sana wa kanisani 🙏 naamini ipo siku nitafanya gospel na kuwabariki wengi kwa mamlaka nilopewa na MUNGU," aliandika Nandy kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii.

Ikumbukwe Nandy amekuwa akifanya Cover za nyimbo za baadhi ya wasanii wa nyimbo huku mashabiki wakimtaka ageukia huko huku wengine wakidai anawazidi wenye nyimbo zao.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger