Mmiliki wa Jamii Forums Maxence Melo Apata Tuzo ya Kimataifa ya Uhuru wa Habari

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


JamiiForums tunampongeza Mkurugenzi wetu Mkuu, Maxence Melo @macdemelo kwa kutangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya Kimataifa ya Uhuru wa Habari (International Press Freedom Award 2019) inayotolewa na Kamati ya Ulinzi kwa Wanahabari (The Committee to Protect Journalists)

Maxence amekuwa mstari wa mbele kupigania haki ya Watanzania kupata na kutoa taarifa kwa zaidi ya miaka 10 kupitia JamiiForums na hata kupelekea kukabiliwa na kesi zinazoendelea hadi sasa

Kila mwaka CPJ hutoa tuzo kwa wadau wa habari wenye dhamira ya dhati katika kuhabarisha jamii zao na hata ikibidi kuweka maisha yao hatarini wakikabiliwa na vikwazo vya kisheria kama kesi, mashambulizi ya kimwili, vitisho, kukamatwa kutokana na kazi zao lakini wakaonesha ujasiri wa kuendelea mbele

Maxence amekuwa Mtanzania wa kwanza kushinda tuzo hii tangu zianzishwe mwaka 1996. Tunajivunia kuwa na kiongozi mwenye msimamo thabiti na nia ya dhati ya kuboresha tasnia ya uhabarishaji hususani mtandaoni

Tunamtakia kila la heri katika harakati za kuendelea kupigania haki ya kutoa na kupokea taarifa na kuahidi kuwa timu yote ya JamiiForums iko naye bega kwa bega katika safari hii


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad