Sakata la Nape na Kinana Lamuibua Kubenea Ainyooshea Kidole TCRA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mbunge wa Ubungo kupitia (CHADEMA) Saed Kubenea, ameiomba Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA), itoe taarifa sahihi juu ya nani aliyefanyakazi ya kusambaza sauti mbalimbali katika mitandao ya kijamii hivi karibuni zikisikika sauti zinadhaniwa kuwa ni za Nape akizungumza na Kinana.

Hayo ameyabainisha leo Julai 22, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar Es Salaam.

Kubenea amesema kuwa lazima faragha za watu ziheshimiwe, kwa sababu nchi hii inawatu wengi wakiwemo mabalozi wanaowakilisha nchi mbalimbali hali anayodai huenda ikaweza kuiingiza TCRA katika mgogoro wa kufungiwa na shirika la mawasiliano la kimataifa.

''TCRA itoe taarifa sahihi juu ya nani aliyefanya kazi hiyo, kama Kinana na Nape amerekodiwa nani ana uhakika kama balozi wa Marekani hajarekodiwa, balozi wa Uingereza hajarekodiwa, viongozi wetu wa vyombo vikubwa hawajarekodiwa, kama wamerekodiana wenyewe kwa wenyewe sisi vipi, wengine vipi, tuache huu utamaduni'' amesema Kubenea.

Aidha Kubenea ameongeza kuwa, kuna baadhi ya sauti zinazosadikikia ni za Makamba akiongea na January, hivyo TCRA inalojambo la kueleza ni nani anayefanyakazi ya kuwarekodi na hofu yake ni kwamba watu hawa wameanza kufuatiliwa muda mrefu, na vipi zikivuja sauti zinazoonyesha wanaongea na nyumba ndogo, inaweza kuleta mtafaruku katika familia zao.

''Wale wanaorekodi hawaedit, wanaedit wanavovitaka wao  pengine kuna mengine mazuri tu yakutaka kumshauri Rais, kama wanataka basi waachie vyote tusikilize siku nzima, watu wanafaragha na ni lazima faragha zilindwe sio vitu vinatolewa tu part 1, 2,3,5 imekuwa kama movie sasa''. amesema Kubenea.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kweli wewe ni Saidi kubenea.
    mie nilifikiri utauliza ya kwako iiyevuja huko chamaani kwenu.

    wewe unataka haya ya wasaliti wa chama kingine.
    Nakushauri ngoma hii mwachie acheze mwenyewe Unaijua SINDIMBA...!!!

    usipigwe Mtama chali..imevujaaaaaa!

    ReplyDelete
  2. Kweli wewe ni Saidi kubenea.
    mie nilifikiri utauliza ya kwako iiyevuja huko chamaani kwenu.

    wewe unataka haya ya wasaliti wa chama kingine.
    Nakushauri ngoma hii mwachie acheze mwenyewe Unaijua SINDIMBA...!!!

    usipigwe Mtama chali..imevujaaaaaa!

    ReplyDelete

Top Post Ad