UFARANSA: Jogoo Ashtakiwa kwa Kuwika, Ajizoelea Umaarufu Baada ya Kufikishwa Mahakamani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Jogoo huyu ambaye mmiliki wake amempatia jina la Maurice, amekuwa kero kwa majirani kwa kuwika kila alfajiri na malumbano kumhusu sasa yanajadiliwa katika mahakama moja nchini Ufaransa.

Analaumiwa kwa kusababisha kalele na familia moja katika kisiwa cha Oléron huko Ufaransa.

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Mmiliki wake, Corinne Fesseau, anasema jogoo Maurice anafanya kile majogoo wote wanafanya ‘kuwikaa’.

Waliomshtaki Maurice na Maurice mwenyewe hawakufika mbele ya mahakama ya mji wa magharibi wa Rochefort siku ya Alhamisi kesi ilipoanza kusikilizwa.

Lakini jogoo huyo ambaye amekuwa maarufu kutokana na kesi inayomkabili, amepata uungwaji mkono kutoka kwa wafugaji kuku wengine ambao walikusanyika nje ya mahakama.

Walalamishi, Jean-Louis Biron na Joëlle Andrieux, walijenga nyumba yao mapumziko katika kijiji cha Saint-Pierre-d’Oléron karibu miaka 15 iliyopita, lakini baadae wakaigeuza kuwa nyumba ya kuishi walipostaafu.

Sababu moja iliyowafanya kuchagua sehemu hiyo ni utulivu wake lakini tatizo ni kuwa jogoo Maurice, amekuwa kero kwao kwani amekuwa akiwapigia kelele kila aalfajiri anapowika.

Wanasema tatizo hilo lilianza tangu mwaka 2017 jirani yao alipomnunua.

Walipowasilisha lawama zao kwa Bi Fesseau, ambaye ameishi Oléron kwa miaka 35, mabishano makali yalizuka mpaka mzozo kati yao ukagonga vichwa vya habari ulipofikishwa mahakamani.

Bi Fesseau, na majirani zake wengine, walisema hakuna mjadala kuhusu swala hilo – kwa sababu ufugaji wa kuku ni sehemu ya maisha ya vijijini na kwamba hawaelewi kwa nini walalamishi wanaomba jogoo huyo azuiliwe kuwika.

Utatuzi wa mzozo huo unasalia na mahakama ambayo inasubiriwa kutoa uamuzi wa kesi mwezi Septemba mwaka huu.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad