Yanga kuikosa AS Vita, Zahera afunguka

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Klabu ya soka ya Yanga bado haijapata timu ya kucheza nayo kwenye kilele chake cha wiki ya Mwananchi baada ya AS Vita kujitoa kuja kucheza kama ilivyokuwa imepangwa awali

Akiongea na EATV & EA Radio Digital, mratibu  wa Yanga  Hafidh Saleh amesema kwasasa bado uongozi wa juu haujawajulisha timu watakayocheza nayo.

''Mazoezi  yanaendelea  kwa mujibu  wa kocha  mkuu  alivyokuwa  anaelekea  na pia  tunasubiri  mpaka  viongozi waseme  tunacheza  na timu ngani baada ya AS Vita kujitoa'', amesema Hafidh.

Kwa upande mwingine Hafidh ameweka wazi siku ya kocha mkuu wa kikosi hicho Mwinyi Zahera kurejea nchini.

''Kocha mkuu Mwinyi  Zahera anarejea  nchini  siku ya alhamis  kwaajili  ya kuungana  na timu  kwenye siku  ya kilele cha Wiki ya Mwananchi Agosti 4, 2019''.

Zahera ambaye ni kocha msaidizi wa timu ya taifa ya DR Congo alikuwa nchini Misri kushiriki AFCON 2019 ambapo timu hiyo iliishia kwenye hatua ya 16 bora.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad