Paul Makonda "Nitashughulika na wanaume wanaowadanganya wanawake kuwaoa"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam , Paul Makonda amesema atatumia mkutano wa SADC kuuliza nchi zao zinafanyaje kuwashughulikia wanaume ambao wanawaumiza wanawake kwa kuwaahidi kuwaoa alafu wanawaacha.

Makonda aliyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alizungumzia ujio wa Rais wa Afrika Kusini ambaye atafika kesho.

Alisema wanawake wengi wa jiji la Dar es Salaam wamechoka kutapeliwa  kwani wanakuwa na majeruhi moyoni hivyo huwezi kuwaongoza watu wenye kuumizwa.

“Tunampango wa kukutana na wadada wote walioumizwa na ahadi za kuolewa lakini wakaachwa ili kujadiliana kwa kina namna gani ya kuwashughulikia wanaume hao lakini pia tutajifunza pia kwa wenzetu wa SADC sheria zao zikoje na wanafanyaje kuwashughulikia wanaume wadanganyifu,” alisema

Aidha, alisema wanampango wa kusajili na kuweka orodha ya kila ndoa zitakazofungwa katika mtandao lengo ni kuwakamata wanaume ambapo ni wadanganyifu kwa wanawake zao.

“Hii data base itsaidia mwanamke akiambiwa kuwa anaolewa ataingia katika mtandao na kuangalia jina la mwanaume huyo kama ameoa au la  na nyie wanawake mkishaolewa washawishini wanaume waje kusajili vyeti vya ndoa,” alisema Makonda.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad