Paul Pogba akosa penalti ugenini

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Paul Pogba amekosa penalti nne akiicxhezea man United katika ligi ya Premia tangu mwanzo wa msimu uliopita

Penalti iliopigwa na kiungo wa kati wa Man United Paul Pogba iliokolewa huku Man United ikizuiwa na Wolveshampton katika mechi ya kusisimua.

Huku ikiwa magoli 1-1 katika kipindi cha pili , raia huyo wa Ufaransa alichezewa visivyo na Conor Coady na kupewa penalti hiyo kuipiga licha ya kukosa penalti tatu msimu uliopita huku Rashford akifunga goli moja dhidi ya Chelsea katika mechi ya ufunguzi wikendi iliopita.

Shambulio hilo la pogba lilipanguliwa na Rui Patricio ambaye aliruka upande wake wa kulia.


Katika kipindi cha kwanza kilichoshirikisha mashambulizi matatu , Anthony Martial alikuwa ameiweka kifua mbele Man United akiifungia klabu hiyo goli lake la 50 - kabla ya Ruben Neves kusawazisha kupitia shambulio kali karibu na eneo la hatari dakika 10 baada ya kipindi cha kwanza.

Kichwa cha mshambuliaji wa Wolves Raul Jimenez kiligonga mwamba wa goli kabla ya Neves kufunga lakini hakuna kipa aliyevamiwa na mashambulio baada ya Pogba kukosa penalti hiyo.

Wakati mzuri na mgumu wa Martial
Haki miliki ya pichaREX FEATURES
Image caption
Anthony Martial amefunga magoli 36 ya ligi ya Premia akiichezea Manchester United miongoni mwa magoli 50
Akizungumza na vyombo vya habari siku ya Ijumaa, mkufunzi wa United Ole Gunnar Solskjaer alisema kwamba anamtaka Martial na Rashford kufunga magoli wanapokaribia lango la upinzani.

Pengine alikuwa akizungumzia kuhusu krosi iliopigwa na Rashford karibu na mwamba wa goli katika kipindi cha kwanza.

Martial hakusukuma mguu wake mbali na kushikana na beki huyo huku fursa hiyo ya wazi ikipotea.

Kilichofuatia ni magoli mangapi ambayo raia huyo wa Ufaransa anaweza kufunga iwapo atafuata mkondo huo wa kuwa hatari mbele ya lango.

Baada ya dana dana nzuri ilioanzishwa na Jesse Lingard akiwemo Luke Shaw na kumaliziwa na Rashford aliyepiga kombora la chini chini na kupita safu ya ulinzi ya Wolvehampton, Martial alipiga mkwaju kwa haraka huku kipa wa klabu hiyo akikosa nafasi ya kuokoa mkwaju huo.

Ulikuwa wakati mzuri kwa wageni hao ambao waliathiriwa na kupewa kadi ya njano kwa Daniel James kwa kujiangusha.

Kipindi cha pili ilikuwa hadithi tofauti lakini United pengine ingeibuka mshindi iwapo Pogba angefunga penalti hiyo.

Swali kuu ni kwamba ni kwa nini Pogba aliipiga penalti hiyo?
Baada ya kufunga dhidi ya Chelsea , Rashford pia alifunga penalti ya dakika za mwisho na kuipatia ushindi timu yake dhidi ya PSG msimu uliopita mbali na kufunga penalti ya England dhidi ya Colombia katika kombe la dunia la 2018.

Katika kipenga cha mwisho , Pogba alijifunika kichwa chake na tishati yake alipokuwa akitoka uwanjani.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad