Sisemi WCB ni Wanyonyaji, iko Haja Diamond Kujitathimini...Alianza KifesiIlianza kwa Kifesi. Miongoni mwa vijana wa Kitanzania wenye uwezo mkubwa wa kupiga picha, alitangaza kuondoka WCB kupitia Instagram. Sababu ikidai kua anataka ‘kukua zaidi’, lakini baadae dada wa Diamond, Esma akaweka wazi kua, Kifesi alifukuzwa kazi. hakuna aliyejali. Burudani zikaendelea.

Ikahamia kwa Q Boy Msafi; miongoni mwa Designer bora kabisa wa Diamond, nae akatangaza kutoka WCB. Sababu yake ikiwa ni kusaka changamoto mpya, lakini muda mfupi ukweli wa chanzo cha kuondoka ukaja. Huyu kuna siku aliwahi kukaririwa akijutia maamuzi yake. Kuna aliyejali? Hakuna. Kila mtu akaendelea na mishe zake.

Baadae kidogo, Rich Mavoko akaondoka WCB kwa mlango uleule aliouitumia kuingilia. Kwa Rich yakazuka maneno mengi. Moja ikiwemo Diamond kuwapendelea baadhi ya wasanii. Pili ni kuwanyonya kwenye haki zao.

Bahati mbaya Mavoko alikua kama ‘mtoto wa kambo’ pale WCB. Alilalama na hakuna aliyempa sikio la kumsikiliza. Maisha yakaendelea. Now imehamia kwa Harmonize. ‘mtoto wa kwanza’ wa Diamond.

Kijana mwandamizi wa WCB. Alimpenda Diamond, akapendwa na Diamond. Walifanana kwenye kuimba mpaka kwenye mfumo wao wa maisha. Harmonize ameandika barua ya kuomba kuondoka WCB. Bahati nzuri yeye bado hajafungua kinywa kueleza sababu. Wengi wanaamini ni kwa ajili ya kukua kimuziki, lakini kwa maneno ya Salam SK, kuna shida ilikuwepo WCB kati ya Harmonize na uongozi kabla ya kufikia maamuzi ya kuandika barua.

https://kiss100.s3.amazonaws.com/wp-content/uploads/2019/08/Sallam-SK-WCB-records.jpg
Meneja wa WCB, Sallam SK wakati akizungumzia kujitoa kwa Harmonize
Ni wazi hili la Harmonize haliwezi kumuacha salama Mondi. Lina maswali mengi kwa watu wa nje. Sawa, wale wa kwanza ni sehemu ndogo ya WCB, kuondoka kwao ni kawaida, lakini inakuaje na Harmonize anaondoka hivi?

Mbona alitakiwa kupewa heshima, akapewa baraka na akaruhusiwa kukua zaidi! Anaondokaje hivi? Kauli ya Harmonize kama mtoto wa familia, inaweza kuaminisha ukweli uliowahi kusemwa na waliowahi kutoka mwanzo. Sisemi WCB ni wanyonyaji, ila iko haja ya Diamond kama bosi kujitathimini. Iko haja ya Diamond kuitazama upya ofisi yake. ‘Brand’ ya WCB ni kubwa na inatakiwa kwenda tofauti na ilivyo sasa.


Tulitegemea vijana waibuliwe, wakue kisha waondoke kama mabalozi wazuri wa WCB na sio kwa mfumo huu. Ni mbaya sana hii kwa trust ya taasisi.

Imeandikwa na Ali Kamwe

HABARI HIZI ZINAPATIKANA APP YA UDAKU SPECIAL BONYEZA HAPA  

Loading...

Sisemi WCB ni Wanyonyaji, iko Haja Diamond Kujitathimini...Alianza Kifesi Sisemi WCB ni Wanyonyaji, iko Haja Diamond Kujitathimini...Alianza Kifesi Reviewed by Udaku Special on August 23, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.