UGANDA: Asulubiwa kwa kupigiliwa misumari kwenye mikono, Yadaiwa ameponzwa na kofia ya chama tawala

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Kijana mmoja aliyetambulika kwa jina la Baker Kasumba (21), ameshambuliwa na watu wasiojulikana wakati akitoka kazini kuelekea nyumbani katika eneo la Kalerwe, Jijini Kampala siku ya Alhamisi ya Agosti 29, 2019 ya wiki hii.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi mjini Kalerwe,  Imeeleza kuwa Kasumba alikutwa amepigiliwa misumari ya nchi 6 kwenye mikono yake yote katika makutano ya barabara ya Kalerwe.

Taarifa hiyo, inaeleza kuwa kijana huyo alivaa kofia ya Chama cha Tawala cha National Resistance Movement    (NRM) kinachoongozwa na Rais Yoweri Museveni.

Kwenye maelezo yake aliyoyatoa katika kituo kidogo cha Kibe mjini Kampala, Kasumba amesema kuwa wakati akiwa njiani kutoka kazini, Alisimamishwa na watu wawili na kisha walimvua kofia na kumvuta mikono yote miwili na kuanza kumpigilia misumari kwenye mikono yake, Huku wakimwambia ‘Kofia yako imekuponza’.

Polisi nchini Uganda inaendelea na uchunguzi kuwabaini watu hao waliomshambulia kijana huyo, Kwa sababu za kisiasa.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad