Waziri Mkuu Aagiza DED Achunguzwe

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga awasilishe kwake taarifa za utendaji kazi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Waryoba Gunza baada ya kushindwa kutoa maelezo kuhusu utekelezaji wa mradi wa maji kata ya Rutamba.

Ametoa agizo hilo Agosti 23 wakati akizungumza na wananchi katika Mkutano wa hadhara, uliofanyika kwenye kijiji cha Rutamba akiwa katika ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za maendeleo na huduma za jamii mkoani Lindi.

Kwa mujibu wa Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Lindi amesema kuwa mradi wa kata hiyo unakabiliwa na tatizo la uchakavu wa miundombinu na ukarabati wake unahitaji bajeti ya  sh. milioni 75, ambazo wameziomba kutoka Wizara ya Maji.

”Miradi yote ambayo gharama zake ziko chini ya sh. milioni 100 inatakiwa itekelezwe kwa kutumia fedha za ndani ya halmashauri husika, miundombinu hiyo ilitakiwa iwe imebadilishwa, mradi wa sh. milioni 75 unaomba fedha wizarani? huu ni uvivu,” amesema Majaliwa.

Waziri Mkuu amesema suala la huduma ya maji limewekewa msisitizo na Rais Dkt. John Magufuli kwa kuanzisha kampeni ya kumtua mama ndoo kichwani, inayolenga kuwawezesha wananchi kupata maji safi na salama karibu na makazi yao.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad