Zari si Mchezo....Afunguka Kuzaa Watoto Kumi...Uwezo wa Kuwalea Anao

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mwanamama ambaye mfanyabiashara maarufu Zarina Hassan ‘Zari The Bosslady’ amesema anapenda sana watoto na ikibidi anaweza kufikisha idadi ya watoto kumi kama Mungu atamjaalia.

Zari ambaye ni mzazi mwenza wa Diamond Platnumz amesema hayo wakati akifanyiwa mahojiano na mtandao wa Millard Ayo amesema watoto ni baraka kubwa kwani watu wa kizazi kilichopita walikuwa wakizaa watoto wengi na kuleta faraja kubwa wakati kunapokuwa na tukio linalowakutanisha wanafamilia.



“Kwanza natamani kuwa na watoto kumi, unajua watu wa zamani walikuwa wanazaa, ukiangalia familia za zamani mara unakuta watoto kumi. Ukifika wakati wa Christmas kunakuwa na mkusanyiko mkubwa, binamu, nani…..siku hizi ikifika Christmas unakuta katoto kamoja tu..hapana, mimi napenda sana mambo ya asili, nataka watoto kumi.”

Amesema kuzaa ni baraka na zawadi kubwa kutoka kwa Mungu kwani kuna wanawake wengi ambao wanahangaika kupata watoto lakini hawapati.

Amesema kwa kuwa uwezo wa kuwalea wote anao hana sababu ya kuogopa kuzaa.

Zari ameweka wazi ikiwezekana basi mpenzi wake wa sasa ambaye ndiye mume mtarajiwa atamzalia mapacha kama ikishindikana hata kwa njia ya kutumia mama mbadala.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad