Hivi Wanandoa Wenzangu na Wake zenu pia Wako Kama Huyu Wangu?

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Baba yangu mzazi kaja juzi kutoka kijijini kwa matibabu.Nilimkatia tiketi ya ndege akapandie mkoani, mke wangu akadai ni uharibifu wa pesa kumsafirisha Mzee kwa ndege angepanda basi wakati mzee wake mwezi uliopita alikua hapa kwetu na kaja kwa ndege kwa hela yangu wakati haumwi ni mzima na baba yangu alikua mgonjwa.

Kana kwamba hiyo haitoshi mizunguko yote ya muhimbili naenda mm na ndugu zangu Wa ukoo yeye yupo busy na kazi, anaenda kwa kusukumwa mno.

Ukiachana na hilo hata misiba ya ukoo wetu either atatafuta sababu inayokaribiana na ukweli asiende au ataenda akifika pale anageuka mgeni hashughuliki na chochote.

Wazazi wake wakiwepo hapa itakua ni kama wageni wametoka ulaya nitapigiwa simu nije na grant, sijui ninunue jack Daniels kwamba baba anapenda sana hiyo pombe njoo nayo dear.Weekend tuwapeleke wazazi wake beach yaani inakua ni mikiki ndani.

Tofauti na wazazi wangu wakija hakuna kinachoendelea ndani, hakuna mabadiliko ya vyakula wala nini mimi kwa kuepusha shari huwa namwambia baba twende tukale bar maana anatakiwa ale vyakula chukuchuku au vya kuchoma.

Jana usiku baba aliniuliza kuwa huyu mwanamke mlifahamiana muda gani kabla ya kuoana nikamwambia miaka 4 akasema si kweli hakuamini.Nikajiuliza kwa nn baba kaniuliza swali hili.

Hayo yote ni Tisa Kumi hufanya mambo yake ya maendeleo kimya na kwa siri kubwa humtumia mdogo wake wa kiume kufanya hayo yote I.e kujenga kwa siri. Nikiamua kumweka chini kwa utulivu na kumuhoji kikao hubadilika na kuwa vurugu tupu kwamba namfatilia, kwamba simpi nafasi apumue, kwamba mwanaume nina gubu mimi.

Anyway mimi ni mfanyakazi wa shirika la kimataifa, nina masters, wife ana bachelor degree yeye ni banker
Tuna watoto wawili mmoja yupo primary school standard one na mwingine nursery school.

Wakuu nawauliza hivi:-
(1) Hili ni hali ya kawaida kwa ndoa zote?

(2) Inawezekana sikumfaham huyu mwanake kwa undani?
(Relationship 4 years) je muda huo hautoshi kumjua mtu? Au alificha?

(3) Nimuite mzee yupi kuja kuzungumza nae maana wazee wote wa ukoo wangu anawaona hawana maana

(4) Kuna yeyote kati yenu ndugu zangu wana JF mwenye shida kama hili? Na aliitatuaje?

(5) Wazazi wangu wamechoka na hali hii niwaeleze nini wanielewe?

(6) Nimfanyeje mwanamke huyu?

Naomba ushauri wenu kwa dhati ya moyo wangu maana mimi mwenyewe nimechoka na hali hili iliyodumu kwa miaka 8
Sasa nafikiria REGIME CHANGE

NB: Sijawahi kuchepuka ila kwa sasa ndo nimeanza kufikiria replacement

By didier kinuani/JF
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. nitafute nikushauri esha5552001@yahoo.com

    ReplyDelete

Top Post Ad