9/10/2019

Prezzo Ajitupa rasmi kwenye siasa

Msanii wa muziki wa Hip Hop nchini Kenya, Jackson Makini almaarufu kwa jina la Prezzo ametangaza rasmi kuingia kwenye siasa kwa kuchaguliwa nafasi ya kugombea ubunge katika jimbo la Kibra nchini humo.Prezzo ameteuliwa na Chama cha Wiper leo Jumanne Septemba 10, 2019,  mbele ya kiongozi wa Chama hicho,  Kalonzo Musyoka ambaye alishawahi kuwa makamu wa Rais wa Taifa hilo.

Taarifa hiyo imepokewa na kwa mikono miwili na Wakenya, Huku wengi wakimlinganisha na msanii mwenzie wa muziki, Jaguar ambaye yeye kwasasa ni Mbunge wa Jimbo la Starehe.

Kalonzo anaamini kuwa kutokana na ukumbwa wa Prezzo,  Anauwezo mkubwa wa kuchukua jimbo hilo kwenye uchaguzi utakaofanyika Novemba 7 mwaka huu.

Prezzo atapambana na mwakilishi mwingine wa Chama cha ODM, Imran Okoth kwenye kinyang’anyiro cha kusaka ubunge kwenye jimbo hilo la Kibra.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger