9/21/2019

RC Ally Hapi Amtupia Dogo Baya Msigwa "Ukitumia Kiinua Mgongo Utaumia"


Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi, amewatumia salamu viongozi wa upinzani akiwemo Mbunge wa Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa kuwa, pesa zake anazolipwa na Bunge asithubutu kuzitumia wakati wa kampeni za uchaguzi kwani atazipoteza bure.

Hapi ameyabainisha hayo leo Septemba 20, wakati wa ufunguzi wa maonesho ya kitalii ya nyanda za juu Kusini yenye kuhamasisha watu kutembelea kanda hiyo na kujionea vivutio vilivyopo na kusema kuwa mkoa huo tayari umekwishajengeka kutokana na uboreshaji wa miundombinu uliofanywa na Serikali ya awamu ya Tano.

''Ndugu zangu wapinzani akiwemo rafiki yangu Msigwa, wawe na tahadhari kubwa kwenye kutumia viinua mgongo vyao watakavyopewa na Bunge, wasije wakathubutu kwenda kwenye uchaguzi kwa kutumia viinua mgongo mtakavyowalipa Bungeni kwa sababu watajitafutia sukari, presha na magonjwa mengine nyemelezi, chuma Dkt  John Magufuli amefanya kila kitu, sasa wewe unachukua kiinua mgongo kwenda kwenye uchaguzi mtapoteza'', amesema Hapi.

Aidha Hapi ameongeza kuwa viongozi wa kanda ya Kusini kwa pamoja wamejipanga ili kuhakikisha utalii unakua kwa kasi na kwamba hawatoweza kumuangusha Rais Magufuli.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger