10/05/2019

Baada ya Kujitoa WCB Sasa Harmonize na Zari Mambo Motomoto

YAPATA zaidi ya mwezi mmoja sasa tangu ilipofahamika rasmi kwamba, supastaa wa Bongo Fleva; Rajab Abdul Kahali ‘Harmonize’, amejitoa kwenye lebo ya muziki iliyomlea ya Wasafi Classic Baby (WCB) iliyo chini ya mwanamuziki Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’.

Hata hivyo, tukio hilo lingali bado linatrendi, kuna mengi nyuma yake huku kila mtu akisema lake, lakini kubwa ni ukaribu motomoto ulioibuka kati ya Harmonize au Harmo na eksi wa Diamond au Mondi; Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.

ZARI DUBAI
Akiwa Dubai kwenye bata ndefu wakati wa birthday yake mwishoni mwa wiki iliyopita, Zari alirekodiwa kipande cha video akiimba na kucheza wimbo mpya wa Harmo wa Inabana alioshirikiana na mwanamuziki wa Uganda, Eddy Kenzo.
Si unajua tena zile mbwembwe za Zari? Yaani tukio kubwa la birthday ya mama watano lipite hivihivi bila kujulikana?

ATUPIA NUSU UTUPU
Basi unaambiwa akiwa kule Dubai ndipo akawa anafanya mambo kibao ya kusababisha vichwa vya habari kama kukaa na kutupia nusu utupu kisha kurekodiwa video na kusambazwa mitandaoni.

“Wewe mama mtu mzima, mama wa watoto watano umekaa uchi, unadhani wanao wakikuona…. (tusi), wanakuchukuliaje?” Ilisomeka sehemu ya maoni lukuki ya video na picha zake za utupu mtandaoni.

Hata hivyo, kufuatia mashambulizi aliyopewa, Zari naye aligeuka mbogo na kujibu mapigo kuwa hayawahusu na kwamba hayo ni maisha yake.

HARMO SIFA LUKUKI
Baada ya hapo ndipo sasa Zari akatupia shangwe kama lote akiimba na kucheza wimbo huo wa Inabana wa Harmo huku akimmwagia sifa lukuki.

Baada ya hapo, Eddy Kenzo aliyefanya wimbo huo na Harmo alichukua kipande cha video ya Zari akiimba kisha akatupia kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo mwanamama huyo alimfungukia; “Love the song!” akasindikizia na makopakopa kumaanisha upendo.

ANAMRUSHA ROHO MONDI?
Baada ya hapo kilichofuatia ni mvua ya matusi iliyomshukia Zari huku akiambiwa kwamba bado anamuwaza Mondi ndiyo maana anamsifia Harmo ili kumrusha roho.
Hata hivyo, kwa mara nyingine, Zari ambaye anajulikana kwa kujibu mapigo aliingia kwenye ukurasa wake wa Insta Story na kufunguka; “Wenye mapovu ongezeni… (akataja jina la sababu) kidogo… nguvu zaidi.” Halafu akaweka emoji ya kucheka!

Gazeti hili linafahamu kwamba, siyo mara ya kwanza kwa Zari kujirekodi akisikiliza na kucheza nyimbo za Harmo ambapo hivi karibuni alifanya hivyo kwa nyimbo za jamaa huyo kama Never Give Up, Aiyola na Kwangwaru.

Pia gazeti hili linafahamu kuwa, miezi kadhaa baada ya Zari aliyezaa watoto wawili na Mondi kutengana Februari 14, mwaka jana, Harmo alikaririwa akisema kuwa alitamani kuwaona wawili hao wanamaliza tofauti zao kwani wana mchango mkubwa kwenye kazi yake ya muziki.

TUJIKUMBUSHE
Hivi karibuni, Harmo aliondoka rasmi Wasafi na kwenda kuanzisha himaya yake ya Konde Gang ambapo amekuwa akisapotiwa na Zari kila anapoachia ngoma mpya.

Kwa upande wake, Zari, baada ya kutengana na Mondi miezi kadhaa baadaye alitangaza kuwa na mchumba kisha kuolewa na jamaa ambaye amekuwa akimtambulisha kwa jina la King Bae na kumficha sura kuhofia nyakunyaku.

Naye Mondi, baada ya kutengana na Zari alianzisha uhusiano na mtangazaji wa Kenya, Tanasha Donna Oketch ambaye wanaendelea kujenga familia yao.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger