Breaking News: Wambura wa TFF Aachiwa Huru Akubali Kulipa Milioni 100


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Wambura, baada ya kuingia makubaliano na Jamhuri ya kulipa zaidi ya TSh milioni 100 ambazo alijipatia isivyo halali.Wambura atazilipa fedha hizo kwa awamu tano na  kwa masharti ya kutofanya makosa yeyote kwa kipindi cha miezi 12, ambapo leo amelipa Tsh milioni 20.Hii imekuja baada ya Wambura kumuandika barua kwa Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) kwa ajili ya kuomba msamaha na kukiri makosa yanayomkabili mahakamani hapo.


 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE