10/12/2019

Kaburu, Kabendera wamwandikia barua DPP


Aliyekuwa Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na Makamu wake Godfrey Kaburu, Mwandishi wa Habari Erick Kabendera,  wameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa wameanza majadiliano na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) ya namna ya kumaliza kesi zao.

Hayo yalibainishwa mahakamani hapo kwa nyakati tofauti mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizile ambapo Wakili Jebra Kambole alieleza kwa niaba ya Kabendera.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alidai kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi haujakamilika.

Baada ya Wankyo kueleza hayo, Wakili wa utetezi Kambole aliijulisha Mahakama taarifa ya mteja wake kuandika barua  kwa mujibu wa kifungu namba 194A(2) cha sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kama ilivyofanyiwa mareje mwaka 2019.

Akijibu Wakili Wankyo alidai ni kweli jambo hilo limefanyika na kwamba  Kabendera ameandika barua na ipo katika mchakato na watakapokuwa wamekamilisha wataitaarifu Mahakama.

Baada ya kusikiliza hoja hizo, Hakimu Rwizile aliahirisha Kesi hiyo hadi Oktoba 24, kwa ajili ya kutajwa. Na kama kutakuwa na chochote kabla ya tarehe Jamhuri wataiarifu Mahakama.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger