Magufuli "Watu 138 Wameomba Msamaha Kwa DPP"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Magufuli amesema hadi leo Jumamosi Oktoba 12, 2019 watu 138  wanaodaiwa kuwa na mashtaka ya uhujumu uchumi  wameomba msamaha kwa mkurugenzi wa mashtaka (DPP)  huku nyaraka za wengine 500 zikiendelea kuchambuliwa.


Magufuli ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Oktoba 12, 2019 mjini Mpanda wakati akizindua safari za ndege kutoka Dar es Salaam kwenda mkoani Katavi.


Amesema kulikuwa na watuhumiwa 700 walioomba msamaha.

“Leo nilikuwa nazungumza na DPP kuhusu taarifa za watu waliotubu. Mpaka leo wamefikia 138, wamesharudisha baadhi ya mabilioni ya fedha,” amesema Rais Magufuli.
 “Walioachiwa wako huru wamekwenda kujumuika na familia zao. Huo ndiyo upendo wa pekee kwa sababu tulitoa msamaha na wao wamepokea na sisi tunashukuru. Hao sasa ni raia wema wahesabike kuwa ni raia wema katika nchi yetu.”


Ameongeza, “Nao wataendelea kuachiwa kadri watakavyokuwa wakirudisha fedha, hizo fedha  zitatumika kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania.”
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad