Ndugai Ataka Wanawake Uchaguzi Serikali za Mitaa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Spika wa Bunge, Job Ndugai akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kuhusu semina ya wajumbe wa Chama cha Wabunge Wanawake wa Mabunge ya Nchi Wanachama za Jumuiya ya Madola utakaofanyika jijini Arusha kuanzia 26-29 Oktoba mwaka huu.

KUELEKEA uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24 mwaka huu, Spika wa Bunge, Job Ndugai,  amewataka Watanzania kuwaamini wanawake na kuwachagua ili waweze kuwatumikia.

Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dodoma alipokuwa akitoa taarifa ya semina iliyoandaliwa na Chama cha Wabunge Wanawake wa Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola.


Amesema semina hiyo itafanyika kuanzia Oktoba 26 hadi 29 mwaka huu jijini Arusha ambapo lengo lake ni kuhamasisha wajumbe wake kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu wanawake hususani katika eneo la uchaguzi.

Semina hiyo itakuwa na washiriki takribani 50 kutoka nchi 18 za Jumuiya ya Madola ambapo Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan,  anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.


Ndugai akiwa na  Naibu Spika, Dk Tulia Ackson (kulia) na Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai

“Kauli mbiu ya semina hii ni kuboresha ushiriki wa wanawake katika michakato ya uchaguzi ambapo pamoja na mambo mengine ni kuboresha ushiriki wa wanawake katika michakato ya uchaguzi na hatimaye kuongeza idadi yao katika vyombo vya maamuzi hususani Bunge.

‘Tunafahamu zipo changamoto nyingi ambazo zinakwamisha wanawake kushiriki katika michakato ya uchaguzi kama wapiga kura na wagombea, changamoto hizo zote zitajadiliwa katika semina hiyo,” Amesema.

Aliongeza kwamba wanatarajia kuwa na wageni mbalimbali katika siku hiyo ya ufunguzi wakiwemo Spika wa Bunge la Afrika Mashariki, mabalozi wa nchi 17 za Afrika ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya Madola, Balozi wa Uingereza nchini, Balozi wa Pakistan nchini, mawaziri na viongozi mbalimbali wanawake, viongozi wa dini, baadhi ya watendaji wa serikali za mikoa na wilaya na wawakilishi kutoka UN Women nchini.

“Wanawake wana uwezo mkubwa sana wa kiuongozi, wengi waliopata nafasi walionyesha uwezo walionao. Ni matarajio yetu tutafikia asilimia 50 kwa 50 ndani ya Bunge kama tutaendelea kuwaamini, siyo bungeni tu hadi kwenye vyombo vingine vya kimaamuzi.

“Uchaguzi unaokuja wa serikali za mitaa ukatumike pia kuchagua viongozi walio bora hasa kwa kuzingatia nafasi ya mwanamke kwenye uongozi, tuwaamini wanaweza,” amesema.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad